Naibu Katibu Mkuu CHADEMA na Mbunge wa Kibamba John Mnyika .
Nyumba namba 34 iliyojengwa katika kitalu (block) namba 2 iliyopo Bunju B
mtaa wa kihonze maarufu kwa Ferous, wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es salaam inayomilikiwa na aliyekuwa mbunge wa Kisesa
na mkurugenzi wa uenezi wa muda mrefu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA, Bwana ERASTO TUMBO, kesho jumapili tarehe 2.10.2016 saa nne asubuhi inapigwa mnada kufidia
deni la milioni 300 alilokopa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Tanzania Bara John
Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Kibamba kuwakilisha chama hicho, Jamvi la Habari
limeelezwa.
Moja ya Nyumba iliyomdhamini Mnyika kukopa.
Taarifa za uhakika ambazo Jamvi la Habari linazo zinasema
kuwa tayari mawakala wa kukusanya madeni wa Benki aliyokopa mnyika (Tunaihifadhi) kiasi hicho
cha fedha wameshapita kutangaza matangazo ya kuhusu mnada huo na kwamba kesho
saa nne asubuhi mnada utapigwa ili kufidia deni hilo ambalo ni sehemu ya madeni
mengi yanayomkabili mwanasiasa huyo kijana yanayosemekana kumsababishia msongo
mkubwa wa mawazo kiasi cha kushindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo.Erasto Tumbo Mdhamini wa moja ya mikopo anayodaiwa Mnyika.
Akizungumza na mwandishi wetu maalum, mmoja wa viongozi wa
kampuni ya udalali ya kukusanya madeni na minada walopewa kazi ya kukusanya
deni hilo amesema kila kitu kimekamilika na sasa kilichobaki ni kesho kupigwa
mnada tu kwa nyumba hiyo
‘’kama una mteja au wewe mwenyewe ni mteja tafadhali karibu
sana, kila kitu kimekaa sawa, tumemvumilia sana Mnyika na wenzake, tumesumbuana
naye sana Mahakamani, lakini sasa hatimaye kesho tunapiga mnada’’. Alisema
Nyumba hiyo inayomilikiwa na Tumbo, ilitumika kama Dhamana
ili imuwezeshe Mnyika kukopa pesa zaidi ya milioni mia tatu katika benki moja
maarufu hapa nchini na kwamba Tumbo alimdhamini mnyika kwa kuwa ni kiongozi
wake katika chadema na hivyo hakutegemea kama asingeweza kutokulipa mkopo huo
ambao hata hivyo inasemekana mnyika na wenzake hawakuwekeza pesa hizo kwenye
biashara na badala yake kuwekeza kwenye masuala mengine yasiyohusiana na sababu
ya mkopo.
Alipoulizwa na Jamvi la Habari kuwa inakuwaje wapige mnada
nyumba ya mtu ambaye hajanufaika na mkopo huo na wasitafute mali nyingine za
Mnyika alijibu ifuatavyo ‘’Sisi tunafuata makubaliano ya Mkopo kati ya Mnyika
na wenzake dhidi ya benki, na katika mkopo huu dhamana waliyoweka ilikuwa ni
nyumba na kwamba mmiliki wake alisaini kukubaliana na matakwa ya kimkataba
ikiwemo hili la dhamana kutumika kufidia, sasa aliowadhamini wameshindwa kulipa
hakuna jinsi zaidi ya kupigwa mnada tu’’. Alisema
Uchunguzi uliofanywa na Jamvi La Habari unaonyesha kwamba
Mnyika kwa sasa hana tena uwezo wa kulipa deni hilo wala mengine yanayomkabili
yanayokadiliwa kukaribia kufikia bilioni 1 na kwamba kila anapoulizwa na
wadhamini wake huishia kujibu kuwa biashara zimekuwa ngumu na kwamba ana madeni
mengi hivyo kwa sasa amekata tama.
Hivi karibuni viongozi wenzake wa CHADEMA akiwemo kiongozi
wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho walilipotiwa
kuchangishana kumnusuru mnyika kuingia katika kadhia hiyo ya kufilisiwa.
Taarifa zaidi tutawaletea kesho kabla na baada ya MNADA.
Mlipata muda kuongea na Mnyika mwenyewe? Tusaidieni ili hii iwe balanced story
ReplyDeleteEnter your reply...yana ukweli haya maana mmmh!
DeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDelete