Kiongozi wa Wafanyakazi 31 walipunguzwa kazini na benki kuu ya Tanzania bila kufuata sheria mwaka 1993 amempongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Magufuli kwa utayari wake wa kutaka mambo yaende haraka kwa kuwapa mahakama fedha ili kesi ziharakishwe kusikilizwa.
''kwanza tunamshukuru Mungu kwa mapenzi yake, Lakini pia tunampongeza sana Rais wetu kwa kuiwezesha Mahakama kifedha ili shughuli za upatikanaji wa haki ziendelee kwa wakati, kwa kweli tunamshukuru sana''. alisema Magoti akihojiwa katika taarifa ya habari ya Azam Tv na mwanahabari Baruhani Muhuza jana.
wafanyakazi hao wameamuliwa na mahakama ya rufaa Tanzania kurudishwa kazini na kipindi chote kuhesabika walikuwa kazini na hivyo kupatiwa stahiki zao zote.
mpaka sasa ni wafanyakazi 15 tu kati ya 31 walianzisha shauri hilo ndio wenye uwezo wa kufanya kazi ikiwa watarudishwa wengine wakiwa wamefariki na wengine wagonjwa.
No comments:
Post a Comment