wenyeviti wenza wa UKAWA freeman Mbowe wa CHADEMA Kushoto, Prof. Ibrahim Lipumba wa CUF katikati na James Mbatia wa NCCR-MAGEUZI kulia .
Anaandika NJANO TANO
Tunakumbushana tu, tufanye siasa ndani ya nchi yetu, vyama
vyetu kwa kuongozwa na haja ya kutaka kuleta mabadiliko katika jamii ya
kitanzania na si kwa lengo la kutibu njaa ambayo twajua tiba yake ni
kifo tu,,,, chakula ni dawa tu ya kutuliza maaumivu....
Ni njaa pekeee ndio inayo fanya wasomi na watu wenye akili
timamu kukanyaga misimamo yao bila kuzingatia taratibu au miiko
waliyojiwekea wenyewe!!!! njaa mbayaaa sana!!!!
Ni njaa pekeee,,, ndiyo inayo wafanya watu wamkumbatie
Lowassa mwenye kashfa ya Ufisadi na kuhonga au kununua watu na
KUMKANDAMIZA kabwela Lipumba ambaye pamoja na makosa yake(kama anayo)
watu wanahangaika kumtoa katika uenyekiti kwa kutumia nguvu ya fedha za
Rushwa wanazo zipata kutoka kwa Lowassa badala ya nguvu ya kikatiba na
kanuni walizo jiwekea...
Tunajua,,, CUF chini ya Lipumba ni sawa kabisa na UKAWA
bila CUF, na yule mwenye uchu na uroho wa kuwa rais hawezi kukubali hata
kidogo kuona Lipumba anaendelea kuwa mwenyekitiii......wa CUF.
Lipumba kavunja rekodi, naeza kusema, tumezoea vyama vyetu
kumfukuza kama mbwa mtu wanaye muona tatizo ua kirusi, na huyo mtu
kufukuzika na kwisha kisiasa kabisa!!!
Lipumba sasa unakwenda huu mwezi wa tatu nafikiri,,, bado
wanasumbuana na hao wanao jiita chama, huku hao wajitao chama wakitamba
haikuwahi kutokea mtu akashindana na chama alafu ashinde,,,,,,
Kwa mambo yanavyo endelea, na mgogoro usivyo tabirika,
binafsi nina shaka na hao wanao jiita chama na wanao muita Lipumba
kirusi. Tumezoea virus katika vyama vyetu kutimuliwa siku moja tu,,, na
kisha kwenda kupotelea kwa msajili au mahakaman kama kikimbilia
huko..... mifano ipo,,,,
Lakini kirusi Lipumba aidha kimekuwa sugu kinachoweza
kumuua CUF, au Lipumba si Kirus bali yeye chini ya CUF anapambana
kirusi,,,,.. nani chama hasa chama kati ya Julius Sunday Mtatiro na
Lipumba??? Nani anashindana na CUF kati ya hao???
Sijui,, lakini KUBADILIKA kwa msimamo wa Mtatiro juu ya
kashfa zinazo mkabili Lowassa, na ukizingatia kulikuwa na njaa kanisani
iliyopelekea wachungaji kumuunga mkono Lowassa, na hivyo basi dhahiri
njaa ile sasa iko UKAWA, na njaa hiyo ndio anayo pambana nayo Lipumba.
Vyovyote iwavyo,,, Lipumba andelee kuwa mwenyekiti au
mumtoe kwa kutumia nguvu ya fedha ya Lowassa, bado Lipumba atabaki kuwa
MSHINDI tu, sababu anacho kisimamia kina mashiko, lakini unachokisimaia
Mtatiro hakina mashiko hata kidogo.
No comments:
Post a Comment