marehemu Ashura Mustapha enzi za uhai wake.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi na Mkutano Mkuu wa Chama
cha Wananchi (CUF) Taifa, Mheshimiwa Ashura Mustapha (pichani),
amefariki dunia, leo asubuhi, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa siku chache zilizopita!
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari wa CUFm Taifa,
Mheshimiwa Abdul Kambaya, msiba wa marehemu upo Mburahati eneo la Kwa
Jongo, wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam na mazishi yanatarajiwa
kufanyika kesho mchana, inshaaAllaah.
Ee Mwenyezi Mungu Muumba wa vyote, nakuomba idhini yako
umghufirie, umrehemu na umpe makazi mema ya peponi dada yetu mpendwa,
Mheshimiwa Ashura Mustapha. AMIN.
No comments:
Post a Comment