Na Noel Nguzo.
Wahitimu wa chuo kikuu cha Dar es salaam katika picha.
Mwaka
1966 chuo kikuu cha Dar-es-Salaam kulitokea mgomo mkubwa sana wa
wanafunzi.Mgomo huo uliopelekea jmla ya wanafunzi 400 wa chuo hiko
kufukuzwa kabla ya 392 katiki yao kurudishwa chuoni hapo uliongozwa na
aliyekua kiongozi wa serikali ya wanafunzi wakati huo Samweli Sitta na
marehemu Wilifred Mwabulambo.
Sababu
za mgomo huo unadaiwa kuwa wa kihistoria zilikua ni kupinga kujiunga
na jeshi la kujenga taifa(J.K.T) na kukatwa mshahara,mishahara minono ya
wanasiasa na viongozi wa serikali.
Mwaka
1989 chuo kikuu cha Dar-Es -Salaam ,kulitokea mgomo mwingine mkubwa
uliongozwa na kiongozi wa serikali ya wanafunzi wa chuo hiko wakati huo
Bw Matare Matiko.Katika mgomo huu sababu za wanafunzi kugoma zilikua
;-mauaji ya wafugaji wilayani Kilombero,adha inayotokana na dampo la
uchafu la tabata,ubovu wa kivuko cha kigamboni kilichodaiwa kuharibika
siku mbili baada ya kununuliwa.
Nchini
Kenya mwishoni mwa mwezi septemba kulitokea mgomo katika chuo cha
Multmedia University(M.M.U) chuo hiki kipo kusini mwa Nairobi katika
mji wa Ongata Rongai. Chuo Multimedia University(M.M.U) kipo takribani
kilometa 25 kusini mwa mji mkuu wa nchi hiyo.Sababu ya mgomo huo ni
wanafunzi wa chuo hiko kuungana na wakazi wa mji wa Ongata Rongai
kupinga undeshaji wa hovyo wa madereva wa matatu yanayofanya ruti ya
Nairobi-Ongata Rongai.
Chuo Kikuu cha Dodoma.
Hiyo
ni mifano ya migomo ya baadhi ya vyuo vya nchi nyingine na migomo ya
baaadhi ya vyuo vya hapa nchini ambayo sababu za migomo hiyo ni
changamoto za jamii nzima zinazozunguka vyuo hivyo.Mambo yanaonekana kua
tofauti sana kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini kwa wakati huu.
Kipindi
hiki licha ya jamii nyingi kukumbwa na changamoto nyingi mno,wanafunzi
wengi wa vyuo vikuu hawaonekeni kuguswa nazo.Sisemi migomo ni mizuri au
changamoto zilizopo zitapata utatuzi ikiwa wanafunzi wa vyuo vikuu
watagoma,ninachojaribu kukionesha ni sauti za wanafunzi wa vyuo vikuu
katika changamoto za jamii za kitanzani.Leo ukisikia mgomo chuo flani
basi tatizo ni mikopo tu.Migomo mingi ya wanafunzi wa wakati huu ni ile
inayohusu maslahi yao wenyewe tu basi.
Katika
kipindi cha miaka miwili 2007-2009 nchi yetu ilikumbwa na janga la
mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).Inadaiwa kuanzia mwezi
june 2007 mpaka februari 2009 jumla ya watu wenye ulemavu wa ngozi 43
walidaiwa kuuwawa.Ukubwa wa tatizo ulisababisha tar 4/9/2008 Bunge la
nchi za umoja wa ulaya kutoa tamko la kuridhia juhudi za serikali
kuchukua za kupambana na mauji hayo.Hakuna serikali ya wanafunzi wala
wanafunzi wenyewe kuonesha kuguswa na tatizo kiasi cha kupaza sauti zao
sawasawa.
Nchi
imepita kwenye matukio yenye kugusa maslahi mapana ya taifa kama vile
Buzwagi,sakata la ukwapuaji wa bilioni 306 kwenye akount ya Escrow mwezi
nov mwaka 2014,sakata la Epa,Richmond na hivi karibuni tetemeko la
ardhi lililotokea Bukoba wilayani Kagera tarehe 10/9/2016 na kusababisha
vifo vya watu 16 na wengine kadhaa kujeruhiwa.Hakuna sauti,pole wala
mchango unaokaribiana na hadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu uliofanyika
ilihali mpaka wafanya biashara wa kariako wameshiriki(wanaweza
kujiteteta vyuo vilifngwa) lakini pesa za serikali za wanafunzi zipo
muda wote.
Kasumba
hii ya kuacha kujishughulisha na mambo ya msingi ya jumla jumla nje ya
mambo yao binafsi imeanza kuwaathiri hata wao wenyewe kwa kuanza
kubaguana.Itakumbukwa tarehe 28/mei/2016 zaidi ya wanafunzi 7000
waliokua wanasoma ualimu ngazi ya stashahada maalum ya sayansi
walitimuliwa na serikali.Kama nguvu ya wanafunzi wa vyuo vikuu
wanayoitumia kudai mikipo yao wangeitumia katika sakata lile serikali
isingeweza kuwapa masaa 24 wanafunzi wale waondoke na wala kusingekua na
mwanafunzi aliyelala stand kama ilivyoripotiwa.Kwakua haikua mkopo
halikua jambo muhimu sana kwao.
Nimewahi
kuambiwa kuna chuo kikuu flani mkoani Dodoma kuna bango lenye rangi
na jina la chama cha kimojawapo cha siasa nchini kwenye geti kuu la
kuingilia chuoni hapo lakini chuo hikohiko hakina bango lenye
kukitambulisha chuo hiko unapongia chuoni hapo kama ilivyo kwenye vyuo
vingi duniani.Pamoja na tatizo hili wanafunzi hawaoni kama ni muhimu
sana kuwepo kwa bango lenye jina la chuo kuliko nembo na jina la chama
cha siasa.Wapo kimya kwa sababu sio mkopo.Tarehe 2/6/2016 rais Magufuli
aliwapiga wanafunzi wa vyuo vikuu kuacha siasa mavyuoni,marufuku hii ni
vyema ikaenda sambamba na uondoaji au ukomeshwaji wa alama,au uvaaji wa
sare za vyama ndani au karibu na maeneo ya vyuo.Bango hili la lipo
chuoni hapo mpaka leo ni kwakua sio mkopo.
Kubwa
kuliko yote ni ushiriki wa wanafunzi wa vyuo vikuu katika zoezi la
uchaguzi mkuu.Katika chaguzi kadhaa hasa za mwaka 2010 na mwaka 2015
wanafunzi wa vyuo vikuu wengi walishindwa kushiriki kwenye zoezi hili
kwakua uchaguzli ulifanyika vyuo vikiwa vimefungwa wakati waliandikishwa
mavyuono na ndipo wanalistahili kupigia kura.Husikii wakati huu
wakifanya harakati za kuhakikisha tume ya uchaguzi inatatua taizo
hili,wapo kimya kelele chache wanazopiga vipindi vya uchaguzi zinatosha
kwakua uchaguzi kwao sio mikopo.
Itakumbukwa
kwenye uchaguzi uliofanyika 31/10/2010 katika watu takribani milioni 19
na zaidi waliojiandikisha kupiga kura ni watu milioni tisa na kitu tu
ndio waliojiotokeza huku uchaguzi uliofanyika 25/10/2015 watu zaidi ya
mulioni 23 walijiandikisha lakini waliopiga kura ni watu watu wasiozidi
milioni 16.Ni kweli kwamba sio wote wasiopiga kura ni wanafunzi wa vyuo
vikuu lakini ni ukweli pia sehemu kubwa ya wasiopiga kura ni wanafunzi
wa vyuo vikuu.Katika mazingira ya kawaida kama msomi wa chuo kikuu haoni
tatizo la kutopiga kura kwenye uchaguzi mkuu nini unategemea kwa
wananchi wa kawaida wanoamini katika usomi?
Kimsingi
wanafunzi wa vyuo vikuu wa kipindi hiki kwa kiasi kikubwa kumezwa na
siasa za vyama.Siasa zimeathiri mno wanafunzi wa vyuo vikuu kiasi hata
kuchaguza viongozi wa serikali zao wakati mwingine kunatokana na vyama
wanavyotoka wagombea.Jambo hufanya hata mambo makubwa yanayotokea katika
taifa letu kupokelewa na wanafunzi kulingana na mitazamo ya vyama vyao
au itikadi za vyama hivyo.Wakati mwingine inawezekana ni ubinafsi tu wa
wasomi .
Inawezekana
jibu la baadhi ya wanafunzi ni sheria za chuo zinavyowabana kushiriki
kwenye matukio haya.Kuna baaadhi vya vyuo ni marufku mwanafunzi kuongea
na chombo cha habari au kujitambulisha ni mwanafuzni wa chuo fulani
katika baadhi ya masuala.Lakini mnona hakuna chuo kinachoruhusu migomo
na bado mnagoma mikopo ikichelewa?
Kwa
kipindi cha hivi karibuni wasomi wengi nchini,wanataaluma kwa kiasi
kikubwa wameacha kujishuglisha na mambo ya juma yanayozikumba jamii
zetu.Wengi wameacha usomi wao na kukimbilia kwenye siasa kama sehemu ya
kukidhi mahitaji yao ya kisiasa.Majina mengi yanayotajwa ya
mafisadi,wala rushwa ni ya wasomi.Kwakua walioko mavyuoni hujifunza kwa
wasomi waliomaliza imawezakna wamerithi ubinafsi huu.
Mimi
binafsi kuna wakati niliwahi kukaa na baadhi ya wakazi wa mkoa mmoja
wapo wenye vyuo vingi nikawauliza wananufaikaje na uwepo wa wingi wa
vyuo katika mkoa wao?,walichonijibu faida zaidi ya kuongeza mzunguko awa
fedha kwa kuruhusu biashara nyingi hakuna,wanapenda faida za kudumu
kwakua wakiondoka tu basi na biashara hudorora.Ni wakati wetu sasa
wanafunzi wa vyuo vikuu kushiriki kikamilifu katika changamoto
mbalimbali zinazozikumba jamii zetu.
Imeandikwa na Noel Nguzo.
mwanafunzi chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)
No comments:
Post a Comment