Prof. Kitila Mkumbo, Mwanazuoni Mashuhuri nchini Tanzania.
Siku
za hivi karibuni kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii
kulikua na mjadala mkali sana kuhusu hali ya uchumi katika nchi
yetu.Mjadala huu ulikolezwa zaidi na kauli ya Kiongozi wa kambi rasmi ya
upinzani bungeni Mh Freeman Mbowe kwamba kila mtanzania anadaiwa
takribani milion moja kama sehemu ya mgawanyo wa deni la taifa(trilion
51),Inadaiwa uchumi wetu umedorora na rejea zikitolewa kama kuongeza kwa
deni lataifa kwa miezi kumi toka trilion 49 mpka 51 na kitu(ongezeko la
trilion 2).Kushuka kwa pato la taifa kwa robo ya kwanza ya mwaka 2016
toka 5.7% mpaka 5.5% (tofauti ya 0.2%).
Ni
mjadala huu ulimuibua gavana wa bank kuu na baadhi ya wasomi na "
wachambuzi " wengine wa masuala ya kiuchumi kueleza namna ambavyo uchumi
wetu ulivyo imara.Tatizo ni moja tu inatumika lugha ngumu kuelezea
jambo jepesi.Wasomi wetu wanatumia misamiati migumu sana kubadilisha
tunachokiona,tunachokihisi na tunachoishi.
Kwetu
sisi tuliowengi hatuhitaji maelezo ya kisomi kutambua uwezo wa kifedha
wa serikali,hatuhitaji ma-G.D.P,sijui micro na macro economy, viashiria
vya ukuaji wa uchumi, na lugha nyingine ngumu ngumu.Kinachofanyika sasa
ni sawa na kuelezwa uzuri wa maisha ya nyumbani kwako wakati wajua mara
kenda unazolala na njaa.Sisi tusiosoma tuna maeneo matatu tu ambayo
hutumia kutambua uwezo wa kifedha wa serikali yetu.(.1).HUDUMA ZA
JAMII,(2) MASLAHI YA WATUMISHI WA UMMA,(3) MIUNDO MBINU.
Sisi
tusiosoma hili ni eneo tunalotumia kutambua uwezo wa kifedha wa
serikali yetu.Kudai serikali ina pesa huku tukitambua ubovu wa huduma za
kijamii ni kutogmbanisha na serikali,
Mabadiliko
makubwa ambayo yanaonekana kwenye eneo hili ni mabadiliko ya
kiutendaji, hayana uhusiano wowote na uwezo wa kifedha wa
serikali.Kwamba wakati huu walau kazi zinafanywa,tunaheshimiana kiasi na
ipo nidhamu kwa watoa huduma,japo wengine wanasema ni nidhamu
inayotokana na hofu,jambo la msingi ipo nidhamu.
Lakini
changamoto za msingi zinazotokana na uwezo mdogo wa kifedha wa serikali
zipo au zimeongezeka,ni kweli kwamba bado dawa na vifaa tiba havipo
mahospitalini kama ambavyo ilivyokua wakati wa serikali ya awamu
iliyopita.Wakati huu kuna kelele nyingi kwa sababu wezi wa milion 7 kwa
dakika wamekamatwa,watumishi hewa wameondolewa,ujanja ujanja haupo
banadarini,T.R.A wanavunja rekod za makusanyo kila mwezi,
Hata
huu utamaduni mpya ulioibuka sasa wa kutumia harambee na michango
kutatua matatizo ambayo moja kwa moja ni jukumu la serikali,unatufanya
tushindwe kuelewa mnachotueleza kuhusu uwezo wa kifedha wa serikali
yetu.Tulipaswa kuiona nguvu ya serikali yetu kiuchumi kwenye tatizo la
madawati,tulipaswa kuiona nguvu ya serikali yetu kifedha kwenye tetemeko
la Bukoba.Hawa wafanyabiashara tuliowakwepa kutuchangia wakati wa
kampeni ndo hawahawa tunawakusanya kuwaomba misaada!!
Kuona ni kuamini na bahati nzuri fedha sio hewa, wasomi wetu kuliko kutumia nguvu nyingi kuelezea ni bora mkatuacha tuone.
Hili
ni eneo lingine tunaloweza kuthibitsha uwezo wa serikali
kifedha,Ukiacha ongezeko lilitokana na punguzo la kodi(PAYEE) la 2%
mwaka huu watumishi hawakupata nyongeza ya mshahara ya kila mwaka
(annual increament),kodi za nyumba zinapanda,nauli zinabadilika,ada za
shule zimepanda mishahara imebaki kama ilivyo,hapa unawezaje kueleweka
ukisema serikali ina pesa?
Mpaka
sasa watumishi wengi wenye kustahili kupanda madaraja
hawajapanda,wengine inadaiwa walipandishwa na wakashushwa.Kuna taarifa
zisizothibitishwa kwamba serikali imeamua kuutumia mchakato wa uhakiki
kama sababu ya kutopandisha madaraja,Taarifa hizi zinapewa nguvu na
uweli kwamba uhakiki umechukua mda mrefu sana tena kwa kurudiwa
rudiwa,Serikali ya awamu ya nne ilitumia sana neno "mchakato" kama
sababu ya kupooza mambo magumu,serikali hii inaonekana kutumia mno neno
"uhakiki" katika namna ile ile ile iliyotumiwa nenp mchakato na serikali
ya awamu ya nne.
Serikali
inakuaje na pesa ikashindwa kuajiri? walimu wametosha?vijana
waliomaliza vyuo vikuu mwaka 2015 na 2016 wa taaluma mbalimabli zeney
kuhitajika serikali wapo hawajajiriwa.
Walau
ununuzi wa ndege mbili na ujenzi wa kiwanja cha ndege chato unaweza
kuonekana kama moja ya mambo yenye kuonesha uwezo wetu kiedha,Lakini
hizi ndege wanatumia wakina nani?Kwa nini isiwe barabara ya lami kule
ifakara panapolimwa mpunga?Katika lundo la changamoto za miundo mbinu
tukaamua kuanza na ndege?
Sehemu
kubwa ya miradi na miundo mbinu tulioyonayo wakati huu ni matokeo ya
serikali iliyopita.Serikali ya awamu ya tano bado kupitia miundo mbinu
haijaweza kutuonesha ni kweli makusanyo ya kodi yameongezeka,ni kweli
kulikua na pesa zinapotea kupitia watumishi hewa,ni kweli wanafunzi hewa
na wanufaika hewa wa mikopo waleta hasara zipi.
Ieleweke
hakuna anayetamani kuona serikali inashindwa au kufeli ,ikifeli
serikali tumefeli wote,lakini haukuna sababu kutumia usomi wetu kiasi
cha kutumia lugha ngumu kuelezea mambo mepesi.Uchumi wetu ukiwa sawasawa
hutotohitaji tutangaziwe wala kusimuliwa,tutauona sokoni,tutauiona
hospitalini,tutauona mshuleni,tutauona kwenye mishahara yetu,tutauona
kwenye barabara tutauona,tutaouna,tutauona, tutauona hatutohitaji
uchambuzi kama hu wa sasa
Imeandikwa na Noel Nguzo
simu 0719755055
No comments:
Post a Comment