WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Tuesday, October 18, 2016

DC HAPI WA KINONDONI ACHARUKA, AWASWEKA RUMANDE WATENDAJI WAZEMBE

                                      Mkuu wa Walaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi.
  • Aagiza kuwekwa rumande masaa 24 watendaji 6 wa mitaa, kata na manispaa
  • Ni kwa uzembe na kushindwa kufanyia kazi maagizo yake
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi jana ameendelea na ziara yake katika kata ya Mikocheni ambako ameshiriki kikao cha maendeleo ya kata (WADC), kupokea taarifa ya maendeleo ya kata, kuzungumza na wazee wa kata hiyo na kufanya wa mkutano wa hadhara kusikiliza kero za wananchi.
Katika ziara yake hiyo, Mkuu wa wilaya ameagiza kuwekwa ndani kwa saa 24 Mhandisi wa Manispaa Ya kinondoni kwa kutotekeleza agizo la kufika katika ziara yake kwa wakati ili kujibu kero zinazohusiana na kitengo chake.

Aidha DC Hapi ameagiza pia kuwekwa ndani kwa mtendaji wa kata ya mikocheni na watendaji wa mitaa minne ya Mikocheni kwa uzembe na kutotekeleza maagizo waliyopewa na Mkuu wa wilaya tangu Mwezi Mei Mwaka huu aliyoyatoa katika kikao cha watendaji wa kata za Kinondoni juu ya uanzishwaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi.

Aidha watendaji wa kata hiyo wanadaiwa kupewa fedha za ujenzi wa zahanati na manispaa ya Kinondoni kiasi cha shilingi milioni 42 yapata miaka miwili sasa, lakini bado zahanati hiyo haijaanza kujengwa.
Katika ziara yake hiyo mkuu wa wilaya alisikiliza kero mbalimbali za wananchi ikiwemo uvamizi wa barabara, changamoto za soko la mikocheni na kero ya maji machafu kutiririka kwenye makazi ya watu.
Akieleza dhamira yake katika hatua mbalimbali Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni amepiga marufuku vibanda vya kuonesha video mitaani vinavyochochea utoro shuleni na kuporomoka kwa maadili ya watoto kwa kuonesha picha chafu za ngono.

Mkuu huyo wa wilaya amewasisitiza vionugozi na watendaji wa kata na mitaa kufanya kazi kwa bidii na maarifa na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea.
"Msikae sana ofisini, nendeni mkawatembelee wananchi mjue shida zao na mzitatue. Huo ndio wajibu wetu. Nikipata malalamiko ya wananchi ambayo mmeshindwa kuyafanyia kazi kwa uzembe, mjiandae kuwajibika..." alisema Hapi.

Mkuu huyo wa wilaya leo anaendelea na ziara yake katika kata ya Magomeni.

No comments:

Post a Comment