Mohamed Nyundo.
mwenyekiti wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Pwani (UVCCM) PWANI ambaye pia ni mjumbe wa Halimashauri kuu ya Chama hicho Taifa kutokea wilaya ya Mafia, Mohamed Nyundo amewatolea uvivu vijana wenzake wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema waliokuwa wanabishana mtandaoni kwamba CCM imefanya hujuma katika uchaguzi wa Umeya Manispaa ya kinondoni na kuwataka waachane na hadithi zao za kizamani.
''nyie mkishindwa basi mmehujumiwa, mkienda mahakamani mkishinda kesi basi mahakama imetenda haki, mkishindwa mnasema Mahakama ya CCM na mmeonewa, nyie watu gani hivi''.
Nyundo alionyesha kusikitishwa zaidi na tabia hizo na kuwaambia zama za kujitekenya na kucheka wenyewe zimekwisha na sasa hivi vijana wa CCM kamwe hawataacha waendelee kupotosha kila mara.
''unajua mambo mengine yanachekesha kweli, Kususa mnasusa wenyewe, hivi aliyewaambia mkisusa akidi haitimii nan, kususa kwenu hakuwezi kubadili matokea, mmeshindwa kubalini yaishe jiandaeni na uchaguzi uhao''. amenukuliwa MNEC huyo wa Mafia.
No comments:
Post a Comment