WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Thursday, October 13, 2016

BREAKING NEWS:- DAVID KAFULILA ABWAGWA TENA MAHAKAMA YA RUFAA. SASA KUSUBIRI BUNGE MPAKA 2020

Ndoto za aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini David Zakaria Kafulila kurudi Bungeni katika Bunge la kumi na moja, jana ziliyeyuka katika Hukumu ya kesi ya Rufaa ya uchaguzi kati ya mwanasiasa huyo machachari wa Nccr Mageuzi dhidi ya Mbunge aliyeshinda wa jimbo hilo Hasna Mwilima ambapo Jopo la Majaji watatu lilimtangaza Hasna Mwilima kuwa mshindi wa kesi hiyo baada ya kutokukubaliana na hoja za rufaa zilizowasilishwa na mbunge huyo wa zamani wa jimbo hilo.

katika kuonyesha kuwa Kafulila hakuwa na uhakika wa kushinda rufaa hiyo, hakutokea mahakamani kusikiliza wala wafuasi wake waliokuwa wakimuunga mkono nao hawakutokea mahakamani kama ilivyokuwa kawaida jambo linaloonyesha ni kwamba Kafulila alishakata tamaa.

JAMVI LA HABARI lilikuwepo katika viwanja hivyo vya mahakama na kumshuhudia mbunge Mwilima na wafuasi wake wakifurahia ushindi huo wa mara ya tatu baada ya ule wa jimboni, kisha mahakama kuu na sasa mahakama ya rufaa.

sambamba na hukumu hiyo, kafulila amehukumiwa kulipa gharama zote za kesi hiyo.
JAMVI LA HABARI

No comments:

Post a Comment