WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Tuesday, October 18, 2016

MWIGULU AFAFANUA TUHUMA ZA YEYE KUGUSHI VYETI VYA ELIMU YAKE

Katika Mtandao maarufu wa Jamii Forums, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ametoa ufafanuzi juu ya masuala na minong'ono iliyokuwa ikiendelea juu ya uhalali wa elimu yake.

 Mwigulu Nchemba.
Salama comrades?

Nimeiona thread hii: Mwigulu, Kigwangalla, Makonda jibuni tuhuma hizi nzito, aliyeandika naona hajui historia yangu.

Ni vema kuweka rekodi sawa:
Kwanza anasema nilikuwa nanaitwa Lameck Madelu Mkumbo, sasa moja Lameck sio jina la kinyiramba, na Madelu sio jina halisi la baba bali ni utani kuwa ana ndevu nyingi, yaani ni mandevu, ndio maana hata kwenye ubunge nililiongeza tu kama a.k.a ili watu hasa wazee wanifahamu hili haliko kwenye vyeti.

Hili la Lameck siyo jina la kinyiramba ni jina la daktari aliyenipokea zahanati ya Iliyopo kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo lakini ni Nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu Lameck. Mimi nilipelekwa hosipital nikiitwa Mugulo na jina la ukoo kwa watoto wote wakiume ni Shumbi ambalo hata hivyo wanatumia wazee tu wanaojua kinyiramba hilo ndio jina la kinyiramba. Mama akaulizwa jina akanitaja Nesi yule akamwambia mama unamwitaje jina hilo hakuna lingine mama akamwambia hakuna labda mtaje wewe, basi jamaa akajitaja. Hili lilikuwa jambo la kawaida sana kijijini kwani familia inakuwa na watoto wengi mpaka majina inakuwa sio jambo la kujali sana. Hata pale kijijini kuna wengine waliotajwa majina ya waganga wa kienyeji wazee walikopewa dawa, majina ya manesi/matabibu kama mimi, majina ya walimu nk.

Kuhusu Elimu:
Mimi niliacha shule kwa mara ya kwanza 1984 baada ya kuanza na kaka yangu aitwaye Jugulu, mzee akasema tupeane zamu, nikaacha. Nikaanza 1985, nikaachia darasa la tano nikaenda kuchunga miaka kama miwili. Nikarudi tena baada ya mifugo kuanza kufa sana, mzee akashauri awekeze kwenye elimu. Walimu walikuwa wanashinda nyumbani kumsihi anirudishe shule, ndio nikarudi na nikachukua majina ya daktari. Mtu asichanganye kuona ni udanganyifu, mimi sijachukua vyeti vya mtu. Nimefanya mitihani tena kwa kupiga na picha za passport ili mtu asitumie haki ya mtu mwingine aliyefaulu, na mpaka sasa naona ni struggle za mfano kuwa nilisoma kwa mazingira ya kutoka kuchunga na kurudishwa shule na kufaulu mwenyewe.

Kwa anayetaka kuthibitisha haya anaweza kuwauliza niliosoma nao shule ya msingi.

Comrades, kwa mawazo yangu kosa ni mtu kuchukua nafasi ya mtu aliyefaulu na kwenda yeye, hapo ni kuiba haki ya mtu. Najua hii ilikuwa ikitokea baadhi ya maeneo, mtu anafaulu ila anakuwa hataki kwenda shule au amefariki then anakwenda mwingine. Mimi sijawahi chukua nafasi ya mtu. Halafu watu wanasema jina la mtu, labda kama wanamaanisha tofauti na wizi wa jina kwani kila mmoja hapo alipo ana jina la mtu, yaani atakuwa John wa biblia, Mohamed wa quran, litakuwa la babu, la bibi, la mganga, la daktari, la rafiki, la kiongozi, la tukio nk.

Nijuavyo, jina unakula kiapo tu kama sio la kwako kisheria na unatumia, na hata sasa nikitamani jina jipya nakula kiapo na kutangaza gazeti la serikali na lisipopingwa ndio linakuwa jina langu jipya.

Hoja ni kama mtu kapora cheti cha mtu, kapora nafasi ya mtu mwingine aliyefaulu akaenda kuisomea yeye. But, things do change pia kutokana na nyakati na mazingira

Mwigulu,

No comments:

Post a Comment