WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Tuesday, October 11, 2016

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA JAJI FRANCIS MUTUNGI AZIDI KUPONGEZWA

http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/2756092/medRes/1039429/-/u5mtd2/-/pic+jaji+mutungi.jpg
Pichani Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania Jaji Francis Mutungi akisisitiza jambo. 

HONGERA MSAJILI KUTUNUSURIA CHAMA CHETU

By Saidi Kijangwa.
Nimeyasoma matamko mawili ya Naibu katibu mkuu wa Chama chetu - CUF ZANZIBAR mheshimiwa MAZRUI.  Nimeyasoma kwa makini Sana na Kuna vitu nimejifunza.
Nimejifunza kwamba uamuzi wa Msajili licha ya kusimamia Katiba ya Chama chetu toleo la 2014 lakini umewaumiza Sana viongozi wetu hawa hasa wa upande wa Zanzibar. 

Umewaumiza kwa kuzingatia hoja zao kadhaa zilizoniibulia maswali yanayonifanya nijiridhishe kwamba Msajili yupo sahihi na anastahili pongezi kwa kusimamia tafsiri sawia ya Chama chetu.
Pamoja na hayo nimegundua ifuatavyo. 

1. MAZRUI amenukuu hukumu ya JAJI mihayo - amesahau kwamba JAJI mihayo alitoa hukumu katika kuthibitisha maamuzi halali ya kikatiba,  katiba ikifuatwa kila hatua na hukumu ikatolewa hakuna wa kubishana nayo. 

Kwenye sakata letu hili katiba haikufuatwa,  Prof. LIPUMBA yeye ametumia mapungufu yetu ya kutofuata katiba kutushinda.  na ametushinda Sasa tunaweweseka
Katiba inahitaji kiongozi kuridhiwa kujiudhulu na mamlaka iliyomchagua - hapo hakuna muujiza,  lazima mamlaka hiyo ipewe heshima yake.  Sasa sisi na viongozi wetu hofu ilikuwa wapi?.



Ningekuwa mimi katibu mkuu,  siku nilipopokea barua ya kujiuzulu Lipumba ningeitisha mkutano mkuu maalum kuridhia swala Hilo.  - maalim hakuitisha,  hakuitisha kwa sababu aliuogopa mkutano ule,  aliogopa mkutano usingeruhusu Chama chetu kisiweke mgombea urais na badala yake kimuunge mkono Lowassa tiliyemuimba Fisadi na aliyeshiriki kukwamisha katiba ya wananchi akiwa na CCM wenzie bungeni. 

Anajua mkutano mkuu usingekubali Chama chetu kugeuzwa daraja la mafanikio ya siasa za CHADEMA. 
ona Leo CHADEMA wametutumia kupata mbunge katika jimbo la NDANDA  tuliloliandaa kwa miaka mingi Sana ...ona sisi hatuna hatuna hata mjumbe wa nyumba kumi Kaskazini. 

Ona mgombea wetu wa Mtwara mjini alivyohujumiwa na CHADEMA kwa kuweka mgombea na kumpatia pesa ili amuangushe mgombea wetu ikiwezekana washindwe wote - hata hivyo tulivuka.

2. Kina MAZRUI wanasahau kwamba Msajili alishawahi kuhukumu mapinduzi kama haya kipindi cha nyuma - Rejea Mgogoro wa JIDULAMABAMBASI na CHEYO - UDP. 

3. MAZRUI na wenzake wanasahau mapema Sana,  wameshasahu kwamba baada ya Msajili kupokea malalamiko ya uvunjifu wa katiba,  Msajili aliziita pande zote mbili zinazorumbana? .
MAZRUI amesahau kwamba upande wao uliitwa tarehe 8.9.2016 na upande wa Lipumba uliitwa tarehe 9.9.2016, kama anasahau mapema hivi atawezaje kukumbuka mambo makubwa zaidi? .
Waliwezaje kuitikia wito wa ofisi ambayo wanaona na wanajua maamuzi yake hawayaheshimu? .
Walifata nini kwa Msajili kiasi cha kubeba na documents kibao? . Aache kutuvurugia Chama MAZRUI.
Hata hivyo wanayaheshimu maamuzi ya Msajili hasa katazo la viongozi waliojipachika kutokujiita viongozi wa Chama.  Ndio mana tangu Jana mpaka Leo sijaona tamko lililosainiwa na Mtatiro wala maharagande tofauti na siku kadhaa kabla ya jana.  Hii inaitwa tii sheria bila shuruti. 

4. Wanasema Lipumba atafanya kazi na Nani viongozi wenzie hawamtaki,  mbona hawajijibu Mtatiro atafanya kazi na Nani? . Kama wajumbe wote wa mkutano mkuu kutoka Bara wanamtaka Lipumba,  Mtatiro ni Nani atulazimishe awe yeye? . Kwanini asihamie tu Zanzibar? .

5. Mbaazi ikikauka husingizia jua,  Timu ya Zanzibar imefeli,  MAZRUI kafeli,  maalim Seif kafeli,  Mtatiro kafeli na Lipumba kafaulu.  Wakabidhi Chama mikono salama. 

6. MAZRUI ANAFANYA KAZI YA CHADEMA.  moja Kati ya masikitiko yetu Wana CUF ni namna CHADEMA wanavyopinga kurejea kwa LIPUMBA kitini,  CHADEMA safari hii wanajidai Wana uchungu kuliko sisi wenyewe,  eti wanaumia kuliko sisi - CHADEMA hawa hawa waliotuita mashoga,  CCM B,  waleberali na majina kibao,  Leo wanatuonea sisi huruma? . 

Ina mana kwa CHADEMA Lipumba kwao ni mbaya Sana kuliko FISADI LOWASSA? .
CHADEMA watuachie Chama chetu,  watuachie Lipumba wetu ya kwetu tutaendelea nayo wenyewe na tutayamaliza. 

Nawashauri CHADEMA waongeze nguvu Kwenye kuimarisha UKUTA wao ulioangushwa na upepo mwezi Jana na ambao hautajengwa mwezi huu. 

MWISHO.
Nawashukuru na kuwapongeza Wana CUF wenzangu hasa wa Bara tuliondelea kupigania kufuatwa kwa misingi ya kidemokrasia na katiba yetu hasa ibara ya 117.
Msajili wa vyama ameshaamua,  kilochobaki ni Prof. Kuendelea na majukumu ya ujenzi wa Taasisi na si vinginevyo,  ninajua wapo watakaoomia kwa wivu,  wapo watakaochukia na tupo tunaofurahia haki kupatikana. 

HONGERA Tena Msajili ahsante kusimamia sheria. 

CUF
HAKI SAWA KWA WOTE
Said Mohammed Kijangwa
Mwanachama.

No comments:

Post a Comment