Wanatumia vyombo vya dola kudhibiti, Polisi kwenye uchaguzi
wamekuwa wengi kuliko wajumbe ili wawatie hofu wajumbe na wananchi
waliojitokeza kushuhudia Uchaguzi huo,
imeripotiwa katika Mtandao marufu wa JamiiForums imeripotiwa hivi.
imeripotiwa katika Mtandao marufu wa JamiiForums imeripotiwa hivi.
Freeman Mbowe,
Madiwani wa CHADEMA Manispaa ya Kinondoki kwenda Mahakamani kesho Jumatatu::
Habari kutoka Kwa madiwani na uongozi wa vyama vinavyounda
Ukawa kesho kupanda mahakamani kufungua kwa hati ya Dharura kwa kile
kilichotokea leo kwenye uchaguzi wa meya wa Kinondoni.
kwa utararibu uliofanyika leo kuna ukiukaji mkubwa wa sheria za uchaguzi na ubabe ulikuwa mwingi sana
nimarumaini yetu kuwa mahakama itayenda haki kwa wote. Mwisho wa kunuku
MWISHO WA CHADEMA KULALAMIKA UMEFIKIA
"CHADEMA ilianzisha Operesheni Umoja wa Kupambana Udikteta
Tanzania (UKUTA), hatuwezi kukaa kimya tena, Nyerere alikataza Vijana
kuwa wanyonge na waoga, hakutaka Taifa la watu waoga, na sisi tunasema
mwisho wa uoga umekwisha, tutakwenda Mahakamani kwa sababu kilichotokea
leo kwenye Uchaguzi wa Meya wa Manispaa Kinondoni leo ni uhuni, kanuni
na taratibu zinavunjwa waziwazi".
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa, Dkt.
Vincent Mashinji, wakati akiongea na waandishi wa habari Makao Makuu ya
Chama hicho yaliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam, leo Jumapili
23/10/2016 baada ya Uchaguzi wa kumapata Meya wa Manispaa ya Kinondoni
kuvunjika.
Wanasheria tegemeo wa Chadema Tundu Lissu na Peter Kibatala walipokuwa mahakani na Saed Kubenea Mbunge wa Ubungo - Picha ya Maktaba .
Wanatumia vyombo vya dola kudhibiti, Polisi kwenye uchaguzi
wamekuwa wengi kuliko wajumbe ili wawatie hofu wajumbe na wananchi
waliojitokeza kushuhudia Uchaguzi huo, Polisi wamewazuia kuingia ndani
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa
CHADEMA kushuhudia Uchaguzi huo, vyombo vya habari vinavyoripoti bila
kupendelea upande wowote vimezuliwa kuingia, waliozuiwa kuingia ni
mwandishi wa Mwananchi, Mtanzania na Tanzania Daima, huku wakiruhusu
waandishi wao wa TBC, Uhuru na Mzalendo, unaweza ukaona jinsi nchi
inavyoendeshwa na Serikali ya awamu ya tano.
CHADEMA kimesema hakitakuwa Chama cha kulalamika tena,
watakwenda Mahakamani, watakusanya ushahidi na kudai haki, Mashinji
amesema wameanza kudai Katiba ya Wananchi ndio suluhisho ya kila kitu,
ni Katiba ambayo ni ya Wananchi ambayo ikipatikana mambo kama haya ya
uvunjaji Sheria,kanuni na taratibu katika nchi utakwisha.
Madiwani wa Ukawa walitoka nje ya ukumbi wa kupigia kura
mara baada ya kubainika mbinu chafu zilizokuwa zimeandaliwa ili mshindi
atoke CCM, Wajumbe kutoka nje ya Manispaa ya Kinondoni wameingizwa
kwenye Uchaguzi huo ikiwa ni kinyume na Sheria na taratibu, huku wajumbe
halali wa UKAWA wakitolewa kushiriki Uchaguzi huo, waliotolewa ni Mhe.
Susan Lyimo na Salma Mwasa.
Akiongea Mhe. Halima Mdee amesema watakwenda Mahakamani kwa
kuwa ni ukiukwaji wa sheria, taarifa ya Uchaguzi hutolewa ndani ya siku
7, ili kutafuta wajumbe, kuangalia mkinzano wa kisheria ili mambo
yawekwe sawa, lakini kilichofanyika taarifa imetolewa siku 1 kabla ya
Uchaguzi ili wafanye mbinu zao ovu, Madiwani wapo 34, ili akidi itimie
lazima kura zipigwe 23,lakini wamepiga kura wajumbe 18 tu, huo ni
uvunjaji wa Sheria ndo maana CHADEMA imeamua kwenda mahakamani.
Source : JF
No comments:
Post a Comment