WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Thursday, October 13, 2016

AHADI YA RAIS MAGUFULI KUWALIPA MISHAHARA UHURU YAYEYUKA.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli, anaelekea kushindwa kutekeleza ahadi yake aliyoitoa mbele ya watumishi wa gazeti la  kila siku linalomilikiwa na chama hicho cha mapinduzi la Uhuru la kuwapatia mishahara yao na madeni yao na siku za nyuma ambayo mpaka anakwenda kuwatembelea walikuwa wamefikisha miezi saba bila kulipwa mishahara yao hiyo.
  Rais Dk. John Magufuli na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi.

Katika ziara yake ya kushtukiza, Rais na Mwenyekiti huyo wa CCM aliwasikiliza wafanyakazi hao wa gazeti la uhuru ambapo pamoja na mambo mengine walimlalamikia mwenyekiti wao kutokulipwa mishahara kwa miezi saba mfululizo na kuwaahidi kuwa wangelipwa haraka iwezekanavyo.
  Rais Magufuli siku alipotembelea Ofisi za gazeti la Uhuru.

Kitendo cha Bodi ya wadhamini ya Gazeti hilo iliyokuwa inaendeshwa chini ya uenyekiti wa Adam Kimbisa kujiuzulu kulitarajiwa kuwa ni mwanga wa wafanya kazi hao kuweza kulipwa mishahara yao lakini mpaka sasa hakuna kitu.
‘’leo ni siku ya kumi na tatu tangu mwezi huu wa kumi uanze, na yeye alikuja tarehe 19 mwezi wa jana, mpaka leo hakuna kitu na tunaishi kwa njaa Kali’’. Kinasema chanzo chetu.

No comments:

Post a Comment