WAZIRI MAMBO YANDANI, MH WAZIRI KATIBA NA SHERIA, MPO WAPI HAKI YANGU, INAPOTEA HIVI HIVI HII NI KWELI
Kijana Mussa Tesha, Mwanachama wa chama cha Mapinduzi CCM amelalamika kutelekezwa na kutokujua hatima ya kesi yake ambayo sasa imefikisha miaka mitano mahakamani huku upelelezi ukiendelea kesi ambayo inamuhusisha yeye kama shahidi wa tukio la kumwagiwa tindikali katika harakati za kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la igunga mwaka 2011 uliofanyika kuziba nafasi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Rostam Aziz aliyeamua kujiudhulu kwa kile alichokiita kuchoshwa na siasa uchwara
katika ujumbe wake unaosikitisha aliousambaza kwenye vyombo mbali mbali vya habari na mitandao ya kijamii, Tesha amewaomba watanzania washirikiane kusambaza ujumbe huo mpaka umfikie Rais Magufuli ili pengine haki yake ipatikane.
Huu hapa chini ndio Ujumbe wake
''MH RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI , AWALI YA YOTEE NAKUPONGEZA KWA KAZI NZURI NA UWELEDI WAKO UNAONDELEA
KUTUTENDEA WATANZANIA WANYONGE NA KUTUJALI HONGERA SANA.
NATUNAKUOMBEA
UENDELEE HIVYO HIVYO NASISI WATANZANIA TUNAIMANI NAWEWE NA TUNAKUOMBEA
ZAIDI UENDELEE NA MSIMAMO HUOHUO.
MIMI NAITWA MUSSA C.TESHA KADA WACCM NA NI MTANZANIA,
NILICHOKUWA NATAKA KULIA NDANI YA SEREKALI HII YAKO YA CHAMA CHA MAPINDUZI
CCM NI KUHUSU KESI YANGU,
MNAMO TAREHE 10/9/2011 NILIFANYIWA UKATILI MBAYA NA
KUMWAGIWA TINDIKALI UCHAGUZI MDOGO WA IGUNGA MJINI NIKIWA NATOKEA OFSI
ZA CCM BILA KUGOMBANA NA MTU WALA KUKOSANA NA MTU YOYOTE NILISHANGA
KUVAMIWA NAKUTEKWA KUPELEKWA MWISHONI MWA MJI NABAADAE KUFANYIWA VITENDO
VYA NAMNA HIYOO NA BAADHI WALIOVIFANYA NILIWATAMBUA.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba
NA BAADA YAKUOKOTWA
NA WASAMARIA WEMA USIKU HUO NILITAJA MAJINA BAADHI NA KISHA KUPOTEZA
FAHAMU SIKUJITAMBUA TENA MPAKA KUJA KUJITAMBUA NIKIWA KCMC NAKUTOA
MAELEZO YALEYALE YA AWALI.
MH RAIS NA VIONGOZI INASHANGAZA MPAKA NIMEONA
NIANDIKE UJUMBE HUU KWAKUWA SEREKALI YA AWAMU YA TANO CHINI YA MH RAIS
WETU JOHN POMBE NI SIKIVU NA NINYEPESI KUTATUA MATATIZO YAWANYONGE.
NILIJARIBU KWENDA MAHAKAMANI KUUULIZIA NILIJIBIWA UPELELEZI BADO MH
RAIS UPELELEZI LEO NI MWAKA WA TANO BADO UPELELEZi HAUJAKAMILIKA
WATUHUMIWAA WANGU NAWAONA,
Waziri wa Katiba na Sheria. Dkt. Harrison Mwakyembe.
NAOMBA MH RAIS UGALIE NAHILI
MH WAZIRI MAMBO YANDANI, MH WAZIRI KATIBA NA SHERIA, MPO WAPI HAKI YANGU, INAPOTEA HIVI HIVI HII NI KWELI
NAOMBA KUWAKILISHA .''
Umeeleza Ujumbe huo wa Mussa Tesha.
No comments:
Post a Comment