katika Ukurasa wake wa facebook, meya mstaafu wa kinondoni na meya mtarajiwa wa Ubungo, Boniface Jacob ameandika maoni yake kuhusiana na suala la mgogoro uliojitokeza mkoani arusha kati ya mkuu wa mkoa huo Mrisho gambo na mbunge wa arusha mjini Godbless lema. zaidi soma mwenyewe
SI MARA YA KWANZA SERIKALI YA MAGHUFULI KUKWAMISHA MIRADI ENEO LA WAPINZANI.
By Boniface Jacob
Maoni yangu ni kuwa sijaona jipya juu ya kilichotokea jana Arusha mbele ya Mbunge Godbless Lema.
Hao wakuu wa mikoa na makuu wa wilaya, wamepewa "maagizo
maalum" ya kukwamisha wapinzani katika maendeleo kwa kipindi cha miaka
mitano,na atakaye kwamisha vizuri kama MRISHO GAMBO anapewa promotion.
Hao wakuu wa mikoa na wilaya "wanamafunzo maalum" ya
kuwakosea heshima viongozi wa upinzani kwenye maeneo yao na yeyote
atakayeonekana anawapa ushirikiano wapinzani uhamishwa eneo hilo haraka
sana kama ilivyokuwa kwa FELIX NTIBENDA ili aletwe kiboko ya
wapinzani(mvurugaji)
Mimi simuoni MRISHO GAMBO kwenye tukio lile la jana bali
namuona mheshimiwa Rais John Pombe Maghufuli kupitia mkuu wa mkoa,yaani
MRISHO GAMBO amemkosha sana moyo mheshimiwa Rais,sitegemei kuona
anakemewa bali anapewa nafasi nyingine ya juu zaidi(kavuruga vizuri)
Serikali haijali juu ya kukosa au kupoteza mradi wa
billioni 9 kutoka kwa Bill and merinda gates foundation au Martenity
Africa,nilishashuhudia kwa macho yangu wafadhili wameambiwa waondoe
billioni 3.2 manispaa ya kinondoni kutoka kwenye barua rasmi ya
serikali,(Naibu katibu mkuu ambaye sasa hivi ni katibu mkuu rasmi)
sababu tuh ni kuwapa (kick) wapinzani.
Mheshimiwa Godbless Lema ameivua ngozi ya kondondoo
serikali na kutuonyesha "chui serikali" alivyo,ili wananchi
wasidanganyike tena wakisikia wanaambiwa hapa kazi tu,maendeleo hayana
chama,mara tunajenga nyumba moja tusigombee fito,kauli hizi zote ni za
kinafki.
1.Manispaa ya moshi(WAPINZANI) imekataliwa mradi wa ujenzi
wa stendi na fedha ni zao wamekopa benki,waziri TAMISEMI kaagizwa
asiwasainie wakati mradi kama huo umekubaliwa manispaa ya morogoro(CCM).
2.Manispaa ya bukoba (WAPINZANI) imekataliwa kujenga mradi
wa stendi mpya ya mabasi billioni 5,waziri TAMISEMI amekatazwa
kusaini,Mradi kama huo umekubaliwa Geita kujenga machinjio billioni
16(CCM).
3.Manispaa ya kinondoni imekataliwa kupewa ruhusa ya
kuingiziwa mitambo yenye thamani ya billioni 3.2 ya uchakataji
taka,mpaka walipe kodi,pia katibu mkuu TAMISEMI amegoma kutia saini
barua ya kuruhusu mkopo wa billioni 14 wakati manispaa ya Temeke (CCM)
wamesainiwa mkopo wa kiasi hichohicho cha billioni 14.
This is foreign aids and opposition's projects frustrations.
NASHUKURU KABLA SIJAFA
WATANZANIA WANAZIONA RANGI NA ROHO ZA VIONGOZI WA SERIKALI HII YA CCM
WATANZANIA WANAZIONA RANGI NA ROHO ZA VIONGOZI WA SERIKALI HII YA CCM
Na Boniface Jacob
Meya mstaafu kinondoni.
Meya mstaafu kinondoni.
No comments:
Post a Comment