WADHAMINI WETU

WADHAMINI WETU

Friday, December 30, 2016

MBUNGE CCM AADHIBIWA KUCHOCHEA MIGOGORO

CCM KASULU YATOA ADHABU KWA MBUNGE NA MADIWANI WAKE KWA TUHUMA ZA KUCHOCHEA MGOGORO WA KUMPINGA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI WA KASULU


Na Rhoda Ezekiel- Kigoma,

KAMATI ya usalama na maadili na kamati ya siasa ya Wilaya ya Kasulu imetoa adhabu kwa Mbunge wa Viti maalumu wa Mkoa wa kigoma,Josephin Ngezabuke na madiwani sita wa Halmashauri ya mji wa Kasulu kwa tuhuma za kuchochea mgogoro wa madiwani kumpinga Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu kwamba aondolewe hafai.


Akizungumza na Waandishi wa Habari jana katibu muenezi wa Wilaya ya Kasulu Masoud Kitowe alisema kumekuwa na mgogoro Mkubwa uliodumu kwa miezi mitano wa Baadhi ya madiwani wa Act na CCM waliomuandikia barua Mkurugenzi ya kudai Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Kasulu aondolewe hafai na Chama Cha mapinduzi hakikupatiwa barua hiyo ambayo ingeweza kuwasaidia kujua chanzo cha tatizo nini.

Alisema katika mgogoro huo madiwani wa CCm walio shiriki ni watano na kati ya hao mmoja ambaye ni Seleman diwani wa kata ya Kumnyika amepewa adhabu ya kalipio ambayo ataitumikia kwa miezi 18 kwa kosa na kushiriki kuandika barua ya kumkataa mwenyekiti wa Halmashauri hiyo wakati jambo hilo bado halijajadiliwa katika Kikao cha Chama kwamujibu sisi kama chama tulipo pata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi tuliwaita madiwani walio husika na kupewa onyo.


Aidha kitowe alisema madiwani wanne waliojiorodhesha kwenye barua ya kushiriki kumpinga Mwenyekiti huyo kamati ya siasa pia imetoa adhabu ambayo kwa Mujibu wa Sheria za Chama cha mapinduzi hairuhusiwi kuitangaza hazarani nao watatumikia adhabu hiyo kwa miezi 12.

Alisema Madiwani hao walipo hojiwa walikili mgogoro huo una chochewa na baadhi ya watu ambao ni Diwani wa Kata ya Murusi Steward Zinduse ambae alikuwa akigombea nafasi ya Mwenyekiyi wa halmashauri akashindwa pamoja na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Kigoma Josephini Ngezabuke nao pia wamepewa adhabu ambayo hairuhusiwi kitangazwa kwa mujibu wa sheria na barua walishapewa zinazo elezea adhabu zao.

Sunday, December 25, 2016

PATA SCHOLARSHIP UKASOME CHINA NA ULAYA

NAFASI ZA MASOMO NCHINI CHINA NA ULAYA List of Scholarships in China for African Students

http://d34elvfuwuckt2.cloudfront.net/wp-content/uploads/sites/21/2015/12/U363P886T1D78573F12DT20130826094825-620x350.jpgChinese scholarships for African students, developing countries and international students - undergraduate, masters and PhD

Masters in Research and Innovation in Higher Education (MARIHE) Scholarships for International Students (Erasmus Mundus) 2017/2018

Masters in Research and Innovation in Higher Education (MARIHE) Scholarships for International Students (Erasmus Mundus) 2017/2018The Masters in Research and Innovation in Higher Education (MARIHE) Scholarship Application Period for student intake in August 2017 (Erasmus Mundus Joint Masters Degree Scholarship) is now open. Apply now.
Application Deadline:  28th February 2017, 11:00 p.m., central European time
Offered annually? Yes
To be taken at (country): 
 » Continue reading about: Masters in Research and Innovation in Higher Education (MARIHE) Scholarships for International Students (Erasmus Mundus) 2017/2018  »

Shanghai Government Scholarship for Bachelors, Masters and PhD International Students 2017/2018

Shanghai Government Scholarship for Bachelors, Masters and PhD International Students 2017/2018This scholarship, provided by Shanghai government for international students studying in Shanghai, is in two types: A, B. Type A, exclusively for those who study for Master’s or Doctoral degrees, is full scholarship, including tuition, free accommodation,accident insurance, allowance for living; Type B, only for those who study fordegrees, is partial scholarship, only including tuition accident insurance.
 » Continue reading about: Shanghai Government Scholarship for Bachelors, Masters and PhD International Students 2017/2018  »

Chinese Academy of Sciences (CAS) – TWAS President’s PhD Fellowship Programme 2017 – China

Chinese Academy of Sciences (CAS) – TWAS President’s PhD Fellowship Programme 2017 – ChinaAccording to an agreement between the Chinese Academy of Sciences (CAS) and The World Academy of Sciences (TWAS) for the advancement of science in developing countries, up to 200 students/scholars from all over the world will be sponsored to study in China for doctoral degrees for up to 4 year
Application Deadline: 31st March 2017
Eligible Countries: International
To be taken at (country): China
Eligible Fields of Study: 
01-Agricultural Sciences
02-Structural,
 » Continue reading about: Chinese Academy of Sciences (CAS) – TWAS President’s PhD Fellowship Programme 2017 – China  »

Jiangsu Provincial Government Scholarships for International Students 2017/2018 – China

Jiangsu Provincial Government Scholarships for International Students 2017/2018 – ChinaJiangsu Provincial Government has set up the Jasmine Jiangsu Government Scholarship for international students in order to promote the development of higher education of International students in Jiangsu, to further improve the profile of Jiangsu Education to the world, to highlight the brand of Study in Jiangsu and to make Jiangsu a preferred province for international students to study in. 
 » Continue reading about: Jiangsu Provincial Government Scholarships for International Students 2017/2018 – China  »

UNESCO – Humanity Photo Awards 2017. Funded to the China Awards Ceremony

UNESCO – Humanity Photo Awards 2017. Funded to the China Awards CeremonyThe China Folklore Photographic Association (CFPA) in association with UNESCO, has launched the Humanity Photo Awards; a call to photographers all over the world to document folklore phenomenon extensively and in depth.
Application Deadline: 15th April, 2017
Eligible Countries: All
To be taken at (country): full-online photo contest.
 » Continue reading about: UNESCO – Humanity Photo Awards 2017. Funded to the China Awards Ceremony  »

Apply Now: China Government Masters Scholarships for African Students 2016/2017 – Fully-Funded

Apply Now: China Government Masters Scholarships for African Students 2016/2017 – Fully-FundedBrief Description: The Government of The People’s Republic of China has made scholarship offers to the African Union Commission, through the Department of Human Resources, Science and Technology, to enable African students study in China in the 2016-2017 Academic Year.
Application Timeline: 26th August, 2016 to 9th September,
 » Continue reading about: Apply Now: China Government Masters Scholarships for African Students 2016/2017 – Fully-Funded  »

Schwarzman Scholars Fully-funded Masters Scholarship for International Students 2017/2018 – China

Schwarzman Scholars Fully-funded Masters Scholarship for International Students 2017/2018 – ChinaBrief description: Designed to prepare the next generation of global leaders, Schwarzman Scholars is the first scholarship created to respond to the geopolitical landscape of the 21st Century.
Application Deadlines: 15th September 2016 (annual)
Offered annually? Yes
Eligible Countries: All
To be taken at (country): Tsinghua University,
 » Continue reading about: Schwarzman Scholars Fully-funded Masters Scholarship for International Students 2017/2018 – China  »

Daff-China Scholarship Programme 2017 for South African Agriculture Scholars

Daff-China Scholarship Programme 2017 for South African Agriculture ScholarsApplication Deadline: 10th of June, 2016 | Offered annually? Yes
Eligible Countries: South Africa
To be taken at (country): China
Brief description: The Department of Agriculture, Forestry and Fisheries in partnership with the Nanjing Agricultural University (NAU), are offering a fully-funded postgraduate scholarship to the People’s Republic of China.
 » Continue reading about: Daff-China Scholarship Programme 2017 for South African Agriculture Scholars  »

75 UNESCO/China Scholarship for Developing Countries Students (Under/Postgraduate) 2017

75 UNESCO/China Scholarship for Developing Countries Students (Under/Postgraduate) 2017Application Deadline: 20 May 2016 | Offered annually? Yes
Session Sept 2016 – June 2017
Brief description: The government of People’s Republic of China in conjunction with the UNESCO is offering 25 undergraduate and postgraduate fellowship for developing countries 2017
Eligible Field of Study
Any applicant can choose one academic program and three institutions as their preferences from the Chinese HEIs designated by MOE.
 » Continue reading about: 75 UNESCO/China Scholarship for Developing Countries Students (Under/Postgraduate) 2017  »

MOFCOM Scholarships in China for Developing Countries (Masters & PhD) 2016

Application Deadline: The Economic and Commercial Counselor’s Office (ECCO) of the Chinese Embassy in your country will be open for application until 30th April 2016 | Offered annually? Yes
Brief description: Ministry of Commerce of People’s Republic of China of offering the MOFCOM Scholarships for Masters and PhD degrees to develop talents from developing countries,
 » Continue reading about: MOFCOM Scholarships in China for Developing Countries (Masters & PhD) 2016  »

TTCL YALA KRISIMASI NA YATIMA DAR


Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kushoto) akimkabidhi mmoja wa watoto wa kituo cha yatima 'Yatima Group Trust Fund Mbagala Chamazi mfuko wa unga, . TTCL imekabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali vikiwemo mchele, sukari, mafuta ya kupikia, soda, maji ya kunywa na mbuzi kwa ajili ya sherehe za Siku Kuu ya Chrismass. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Kituo cha Yatima Group Trust Fund Mbagala Chamazi.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (wa pili kushoto) akimkabidhi mbuzi Mkurugenzi Msaidizi wa Kituo cha Yatima Group Trust Fund Mbagala Chamazi. TTCL imekabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali vikiwemo mchele, sukari, mafuta ya kupikia, soda, maji ya kunywa na mbuzi kwa ajili ya sherehe za Siku Kuu ya Chrismass.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (wa tatu kulia) akimkabidhi mmoja wa watoto wa kituo cha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi cha Kimara SUCA maji ikiwa ni moja ya bidhaa zilizotolewa. TTCL imekabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali vikiwemo mchele, sukari, mafuta ya kupikia, soda, maji ya kunywa na mbuzi kwa ajili ya sherehe za Siku Kuu ya Chrismass.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kushoto) akimkabidhi mfuko wa unga Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi cha Kimara SUCA, Evans Tegete ikiwa ni baadhi ya msaada uliotolewa na kampuni hiyo. TTCL imekabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali vikiwemo mchele, sukari, mafuta ya kupikia, soda, maji ya kunywa na mbuzi kwa ajili ya sherehe za Siku Kuu ya Chrismass.

Picha ya pamoja ya baadhi ya watoto kutoka vituo vyote vilivyosaidiwa na viongozi wao.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (wa pili kushoto) akimkabidhi mbuzi mmoja wa watoto wa kituo cha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi cha Kimara SUCA. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho, Evans Tegete. 

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kushoto) akimkabidhi mmoja wa watoto wa kituo cha yatima 'Yatima Group Trust Fund Mbagala Chamazi sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya TTCL kwa ajili ya sherehe za Siku Kuu ya Chrismass.

Picha ya pamoja baada ya shughuli ya kukabidhi misaada hiyo. 

Baadhi ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu wakibeba sehemu ya misaada waliyokabidhiwa na TTCL

SHUHUDIA RAIS DKT. MAGUFULI NA MKEWE WALIVYOSHIRIKI IBADA YA KRISMASI SINGIDA



Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda akimuombea na kumbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Misa ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.
Hapa wakiwa katika sala.
Rais Magufuli na mkewe wakisilkiliza neno
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo mkoani Singida 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo mkoani Singida. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakisalimiana na waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya ibada ya Krismasi 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipunga mkono wakati wakitoka kwenye Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida. PICHA NA IKULU

GEREZA KONGWE LATEKETEA KWA MOTO KIGALI

Gereza kuu la Kigali maarufu 1930
Gereza kuu la Kigali maarufu 1930
Gereza kuu la Kigali maarufu 1930 lateketea kwa moto. kufikia leo jioni moshi inaendelea kutanda. Kilichosababisha moto huo hakikajulikana.
Shughuli za kuzima moto bado zinaendelea huku vikosi vya Askari Jeshi na polisi vikionekana hapa na pale kando kando mwa jengo la gereza hilo.
Hilo Ni gereza linalohifadhi wafungwa wa mchanganyiko wale wa kisiasa na wengine wa mauaji ya kimbari. Miongoni mwa wafungwa wa kisiasa Ni Victoire Ingabire aliyehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela miaka 4 iliyopita Kwa hatia ya kuchochea utengano wa kikabila na kuhatarisha usalama wa raia.
Viongozi kadhaa serikalini wamefika kwenye eneo la tukio wakiwemo mawaziri na wakuu wa jeshi na polisi.
Bado Ni mapema kujua athari zilizotokana na tukio hilo kwani waandishi wa habari hawajaruhusiwa kuingia katika jengo la gereza kuu ya Kigali.
Magari ya zima moto bado yanapishana na magari ya kubeba majeruhi huku wafungwa wakionekana nje ya gereza na ulinzi ukiwa umeimarishwa.BBC

ZITTO KABWE AONGOZA WADAU KUHANI MSIBA WA MPOKI BUKUKU TABATA JANA

Kiongozi wa Chama cha ACT, Zitto Kabwe (kulia) akizungumza jambo na Shemeji wa marehemu Mpoki Bukuku, Edwin Mjwahuzi alipokwenda kuwafariji wafiwa nyumbani kwa marehemu, Tabata Bwawani.


Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mtanzania, Absalom Kibanda akimfariji mjane wa marehemu Mpoki Bukuku, Lilian nyumbani kwa marehemu, Tabata Bwawani, Dar es Salaam. Bukuku alifariki juzi baada ya kugongwa na gari Barabara ya Bagamoyo karibu na Kituo cha ITV, Mwenge. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Kibanda akimfariji mama mzazi wa marehemu Mpoki Bukuku



 Zitto Kabwe (kulia) akizungumza na kaka wa Marehemu Mpoki, Gwamaka Bukuku wakati wa msiba huo

 Waandishi wa habari wakiwa kwenye msiba wa marehemu Mpoki Bukuku ambaye alikuwa Mpigapicha mwandamizi wa magazeti ya Kampuni ya The Guardian

 Wanahabari wakijadiliana mambo wakati wa msiba huo

Mmmiliki wa Blogu ya KAMANDA WA MATUKIO BLOG, Kamanda Richard Mwaikenda, ambaye pia ni Mpigapicha Mkuu wa gazeti la Jambo Lelo, Kamanda Richard Mwaikenda (kulia) akiwa na wanahabari wenzie kwenye msiba huo.Kutoka kushoto ni Mpigapicha wa Waziri Mkuu, Hilary Bujiku, Mmiliki wa Blog ya K-VIS, Khalfan Said, Mmiliki wa Blog ya Michuzi, ambaye pia ni Mpiga Piacha na Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais, Muhidini Issa Michuzi, Mpigapicha Mkuu wa Gazeti la Mwananchi, ambaye ni shemeji wa marehemu Mpoki, Edwin Mjwahuzi na Francis Chirwa ambaye ni mmoja wa viongozi wa Bodi ya Wahariri wa Gazeti la Raia Mwema

BOT YAKANUSHA KUTOTUMIKA NOTI YA SHILINGI 500



Benki kuu ya Tanzania inapenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa,habari inayoenea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba noti ya shilingi mia tano  haitatumika tena kuanzia Desemba 31,2016; sio taarifa ya kweli na ni uvumi unaopaswa kupuuzwa. 

Ukweli ni kwamba noti ya shilingi 500 itaendelea kuwepo katika mzunguko sambamba na ile sarafu ya shilingi 500 hadi pale noti hiyo itakapotoweka mikononi mwa wananchi. Tafadhali mpuuze taarifa hizo sio za ukweli.



Marcian Kobello. 

Mkurugenzi wa Huduma za kibenki- BoT .

LAMECK DITTO : MOYO SUKUMA DAMU

Moyo Sukuma Damu is composed by Lameck Ditto himself and produced by Emma the Boy of Epiq Studios based in Dar es Salaam, Tanzania.The released video, directed by Traveller of Kwetu Studios, is set to achieve massive appeal based on the concept as well as level of detail focused on the project.

Shot in Dar es Salaam, the video will showcase the lifestyle and appeal of the city as a frontier market for music and tourism.Speaking of the release of his video, the talented and well-versed Lameck Ditto said ‘I want to give my fans something they will enjoy to watch as they have enjoyed listening by taking a unique approach to the shootig of the video’.

Follow

Instagram: @lameckditto

Twitter @lameckditto

MPOKI BUKUKU KUAGWA LEO

Baada ya Kupotea:Msako mkali ndege ya Urusi waendelea


Urusi
Rais Vladmir Putin wa Urusi
Msako mkali unaendelea kutafuta miili ya askari wa Urusi walio waliokuwemo kwenye ndege iliyopata ajali kwenye bahari nyeusi iliyoanguka na kuua askri wote tisni na mbili waliokuwemo .
Wafanyakazi zaidi ya elfu tatu, wakiwemo wazamiaji zaidi ya elfu moja wako kwenye harakati za utafutaji manusura ama maiti za askari hao katika eneo la tukio.
Ndege iliyokuwa imebeba askari hao ilianguka dakika tatu baada ya kuanza safari kutoka katika mji wa Sochi ikiwa njiani kuelekea nchini Syria.
Abiria walio wengi walikuwa ni askari wa Urusi waliokuwa katika shamra shamra za sherehe za tamasha la kimuziki la Alexandrov wanaojulikana kama kwaya ya jeshi jekundu.
Ibada ya kuwaombea marehemu hao imefanyika mjini Sochi na miji mingine tofauti tofauti kabla ya siku maalumu ya Jumatatu iliyotangazwa kuwa ya maombolezo.
Mamlaka nchini Urusi zimetoa tamko kuwa zinafahamu fika wapi ilipo ndege hiyo katika bahari nyeusi. Mpaka sasa miili saba ya askari imepatikana .Mpaka sasa hakuna taarifa zozote za kuwepo kwa manusura wa ajali hiyo.
Msemaji wa wizara ya ulinzi nchini Urusi, Igor Konashenkov, amesema kwamba zoezi la utafutaji linaendelea.BBC

Thursday, December 22, 2016

MCHEZAJI WA ZAMANI WA TAIFA STARS ANAOMBA MSAADA KITANDANI


Kiungo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania na Simba Sports iliyokuwa
ikiitwa Senderland ,Athur Mwambeta amewaomba wadau mbalimbali wa mchezo
wa soka nchini na Chama cha Mapinduzi (CCM) kumsaidia kupata
chombo cha usafiri kitakachomtoa sehemu moja mpaka nyingine mara baada ya
kukatwa miguu yote miwili kutokana na maradhi yanayomkabili.



Mwambeta amesema hayo leo jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum na
Globu ya jamii katika hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo amelazwa
katika jengo la Kibasila ward namba 11, ambapo anaendelea na matibabu
mara baada ya kukatwa mguu ijumaa iliyopita.



"Nimeugua maradhi haya pindi tu nilipoacha kucheza mpira hali
iliyopelekea kukatwa mguu wangu wa kwanza mwaka 2015 na mwaka huu ijumaa
iliyopita ndipo nilipokatwa mguu wangu wa pili na kubaki kama hivi
mnavyoniona, kwani siwezi tena kusogea kutoka sehemu moja kwenda nyingine
kama ilivyokuwa awali hivyo kwa yoyote anaeweza kunisadia naomba
ajitokeze " amesema Mambeta.



Amesema kuwa anaomba wadau kumchangia kupitia nambari hii 0714435312 ili
aweze kujikwamua katika changamoto mbalimbali za kimaisha.



Pia alitoa wito kwa wapenzi na wanachama wa CCM kujitokeza kumsadia
kwani wao ni moja ya watu waliokuwa wahamasishaji wakubwa kupitia TANU
mpaka ilipozaliwa CCM walitumia mpira kama sehemu ya hamasa.


 Wachezaji wa zamani wakiongozwa na Kitwana Manara wakimjulia hali,Athur Mwambeta,ambaye amekatwa miguu yote miwili

BAR YA KWETU PAZURI TABATA YAFUNGWA KWA KUTOKUKIDHI VIGEZO.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg1EiJMSo5vRXmV4XZdFdxDB4LkEe0YBUsdZz2ekbFA9NBc_h2GYHXIRakihrJi3PtJO0GPDtHjGDnKXm-noJ1Q7LObHrZ_uVUKfKCCakPtAsPc84JypRhPlv7mqfhidb0Mp1oYFbSO28ex/s1600/IMG_2078.jpg


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
 
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto ameagiza kufungwa kwa ukumbi maarufu wa Starehe ujulikanao kwa jina la Kwetu Pazuri Tabata kutokana na kushindwa kukidhi vigezo.

akizungumza na Globu ya jamii mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku mbili ,Kumbi la Moto amesema kuwa wameamua kufunga ukumbi huo mara baada ya kufanya na ukaguzi na kujiridhisha kuwa haijakidhi vigezo.

"Tumefanya ukaguzi na kumchukua Meneja wa Bar hiyo na kumfikisha kituo cha Polisi Ukonga Stakishari kwa ajili ya kufunguliwa mashataka na baadae kufikishwa mahakamani"amesema Kumbilamoto.

Amesema kuwa mara baada ya kutoka katika kituo hicho ,alifikishwa kituo cha Polisi kati na kukubali kulipa faini ya Milioni mbili na kukukiri makosa ya kufanya kazi ya Night Club bila kuwa na leseni huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.


Aidha tumewaonya juu ya tabia yao ya kupanga viti karibu na barabara jambo ambalo ni kinyume cha sheria za Tanroads, " hivyo  tumeamua tuifunge mpaka hapo watakapo jipanga upya",Kumbi la Moto amesema na kuongeza kuwa kwa muda mrefu watu walikuwa wakilalamika juu ya sehemu hiyo lakini hatua zilikuwa zinachelewa kuchukuliwa, hivyo nimefika katika eneo la tukio na kujionea hali halisi na kuamua kuifunga Bar hiyo.

Aidha katika ziara hiyo pia amekagua ujenzi wa maabara ya Zahanati ya kata ya vingunguti ambayo inatarajia kukamilika hivi karibuni.

NIT YAKUSANYA MAPATO BILIONI 2 ZA ADA

PROF. MBARAWA: ANDAENI WATAALAMU WA KUTOSHA

mba1
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Prof. Zakaria Mganilwa akitoa taarifa ya utendaji wa chuo hicho kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika uzinduzi wa Baraza la Chuo hicho, jijini Dar es Salaam.
mba2
Mwenyekiti mpya wa Baraza la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Prof. Bavon Nchomba akifafanu jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika uzinduzi wa Baraza la Chuo hicho, jijini Dar es Salaam.
mba3
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wajumbe wa Baraza la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), katika uzinduzi wa Baraza jipya la Chuo hicho, jijini Dar es Salaam.
mba4
Wafanyakazi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika uzinduzi wa Baraza jipya la Chuo hicho, jijini Dar es Salaam.

Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), kimetakiwa kuchangamkia fursa za kuandaa wataalam wa kada mbalimbali za usafirishaji wa anga ili kuinua sekta hiyo na kuiwezesha nchi kujulikana Kimataifa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Baraza la Chuo hicho, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa kuzalisha wataalam pekee haitoshi bali ni jukumu la uongozi wa Baraza hilo kuhakikisha wanawasaidia wataalam hao kwa kuwaunganisha na mashirika makubwa ya usafirishaji lengo ni kuwajengea uwezo na kuwatambulisha kimataifa.

“Tayarisheni wataalamu na muwakutanishe na Wakurugenzi wakuu wa Makampuni kama Emirates, Qatar na Etihad ili kuwawezesha kupata fursa kirahisi na wao kuweza kuonekana kimataifa”, amesema Profesa Mbarawa.
Ameongeza kuwa Chuo kinahitaji kuchukua wafanyakazi kutoka Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), ili kutoa mafunzo kwao kwa ajili ya kuzalisha wataalam wenye ujuzi na uwezo wa kujenga miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Guage).

“Msipotumia fursa kama hizi za kuandaa wataalamu wa mbalimbali, tutakosa watalaamu wazawa wa miradi mikubwa na kuanza kulalamika kuwa Chuo kipo lakini hakithaminiki kumbe mwanzoni tulishindwa kujipanga”, amefafanua Waziri Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amelipongeza baraza lililopita kwa uwezo mkubwa wa kukusanya mapato ya ndani yatokanayo na ada za wanafunzi kutoka Bil. 2.1 kwa mwaka wa fedha 2011/2012 hadi kufikia Bil. 5.1 mwaka 2015/2016.

Aidha, Prof. Mbarawa ameutaka uongozi wa Chuo hicho kuweka mifumo imara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), ili kuweza kuwajengea mazingira mazuri kati ya Walimu na Wanafunzi.
Sambamba na hilo, ameutaka uongozi kupunguza idadi ya kozi zinazotolewa chuoni hapo na kuwa na kozi chache zenye tija na soko kimataifa ili kukifanya chuo hicho kuwa cha kipekee Afrika.
Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa Baraza hilo Prof. Bavon Nchomba amemhakikishia Waziri huyo kushughulikia changamoto zote zinazoikabili chuo hicho kwa kuanzia na upunguzaji wa idadi za kozi zisizo na tija.

Naye, Mkuu wa chuo hicho Prof. Zakaria Mganilwa amesema chuo hicho kitaendelea kuandaa wataalamu mahiri na waliobobea katika Sekta ya Uchukuzi na Usafirishaji na kuomba Serikali kuendelea kusaidia kuboresha miundombinu ya chuo hicho